Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Wahamasika Kushiriki Tamasha la JAMAFEST
Sep 07, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Eleuteri Mangi, WUSM

Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko amesema Watanzania wamehamasika na wamekuja kwa wingi katika Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika kuanzia Septemba 4-12, 2022 nchini Burundi.

Mhe. Balozi Dkt. Jilly amesema hayo Septemba 06, 2022 mara baada ya kutembelea mabanda ya wajasiriamali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioleta bidha zao kwenye hilo.

Nimemaliza kutembelea mabanda ya Tanzania na nchi nyingine, nimeona hamaha kubwa sana, Watanzania wamekuja kwa wingi, watu mbalimbali wameleta bidhaa za sanaa, chakula na kwa sababu Burundi wanapenda sana bidhaa za chakula kutoka Tanzania. Nimeona jinsi wanavyochangamkia mchele, dagaa, viungo vya chakula, mafuta, nguo batiki, mapambo ya mwili na picha za Tingatinga, kwa kweli maonesho yamefana”, amesema Mhe. Balozi Dkt. Jilly.

Mhe. Balozi Dkt. Jilly ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana pamoja na Watanzania ambao wamekuja kwenye tamasha hilo kwa kuwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo Watanzania waishio nchini Burundi, jamii ya kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, wafanyakazi wa mashirika pamoja na kikanda na kuwahimiza kutembelea mabanda yote ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na maonesho hayo ya Sanaa na Utamaduni, mada mbalimbali ziliwasilishwa tamasha hilo ikiwemo jukumu la teknolojia ya kisasa kwa kutumia utamaduni, tasnia ya sanaa na utalii, ushiriki wa vijana katika shughuli za sanaa katika jumuiya ya EAC pamoja na matokeo ya uvumbuzi katika sanaa na utamaduni.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi