Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanaoshindana Michezo ya Afrika Watakiwa Kuipeperusha Bendera ya Tanzania kwa Ushindi
Mar 11, 2024
Wanaoshindana Michezo ya Afrika Watakiwa Kuipeperusha Bendera ya Tanzania kwa Ushindi
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni na wachezaji wa Tanzania wanaoshindana Mashindano ya Michezo ya Afrika (All African Games) jijini Accra Ghana. Machi 10, 2024
Na Shamim Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema, serikali imeendelea kuweka nguvu na mazingira bora kwenye michezo ili kuleta ushindani ndani na nje ya Tanzania hususani Afrika.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Machi 10, 2024 wakati wa hafla ya chakula cha jioni na wachezaji wa Tanzania wanaoshindana Mashindano ya Michezo ya Afrika (All African Games) jijini Accra Ghana huku akiwataka kuhakikisha mbali na kupata ushindi, wanaitangaza Tanzania kupitia sekta hiyo.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia imewekeza fedha nyingi katika michezo katika kipindi hiki, na ni kipindi ambacho Tanzania inafanya vizuri sana kwenye michezo kuliko wakati mwingine. Rai yangu kwenu kila mchezaji acheze kwa kujituma, kusiwe na sababu za kukosa ushindi ambazo hazina mashiko katika mashindano haya", amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuongeza miundombinu ya michezo, wataalamu, vifaa vya michezo, huku akisema kuwa idadi ya washiriki na michezo itaongezeka katika mashindano yajayo.

Katika mashindano yanayoendelea nchini Ghana, Tanzania imepelekea washiriki 109 katika michezo 6 ikijumuisha wanamichezo na watalaamu wa michezo katika michezo ya kriketi wanaume na wanawake, judo, baiskeli, kuogelea, mpira wa miguu wanawake chini ya miaka 20 na ngumi.

Wakizungumza kwa nyakati fotauti wachezaji hao wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kushindana katika michezo hiyo ambayo pia imewapa uzoefu kutoka kwa nchi nyingine pamoja na kupata fursa ya kuitangaza Tanzania kwenye mataifa mbalimbali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi