Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadatoga Wakosoa Ukabila Habari za Ngorongoro
Jun 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff - NGORONGORO

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuacha kuripoti kuwa wanaohamishwa kwa hiari kutoka kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni wamasai peke yao huku vikikumbushwa kuwa eneo hilo linakaliwa na watu wa makabila matatu.

Wito huo umetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Jamii ya Wadatoga Tanzania, Mhe. Augustino Rumay katika Kijiji cha Olpiro kilichopo ndani ya hifadhi hiyo.

“Kwenye vyombo vya habari hata ukienda kwenye mitandao ya kijamii utaona kinachozungumzwa ni jamii moja lakini sisi tunajua sote ni watanzania na tunaishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, lakini ndani ya hifadhi hii kuna jamii tatu zinazoishi humu nazo ni wadatoga, wahadzabe na wamasai.

“Lakini kinachozungumzwa ni kuhamisha jamii moja tu lakini wengine hatutajwi, niwaombe tu wanapozungumzia zoezi la kuhamisha watu ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na sisi pia tutajwe wasiwe wanataja kabila moja,” amefahamisha Mhe. Rumay.

Sambamba na hilo, kiongozi huyo amearifu kuwa jamii ya wadatoga wamehamasika kuhama na idadi kubwa wamejiandikisha ambapo kwa sasa wanangojea awamu yao ya uhamisho ifike.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi