Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vyombo vya Habari Vyaombwa kuelimisha Kuhusu Anwani za Makazi
Apr 27, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Immaculate Makilika – MAELEZO, Katavi

Serikali imeviomba Vyombo vya Habari nchini kuendelea kuelimisha jamii kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi ikiwemo matumizi na utunzaji wa miundombinu ya mifumo hiyo.

Hayo yamesemwa leo mkoani Katavi na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew wakati wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi ambapo amesema kuwa Vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika kuelimisha Watanzania kuhusu  Mfumo huo wa Anwani za Makazi na matumizi yake.

“Serikali inaviomba sana Vyombo vya Habari nchini kuendelee kusaidia kuelimisha Watanzania kuhusu matumizi na utunzaji wa mifumo hii muhimu kwa sababu tumetumia fedha nyingi lakini pia lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia suluhu Hassan la kufikisha kwa wananchi huduma za maji, dharula, afya na mafanikio yake ni mafaniko ya zoezi linalokuja la Sensa ya Watu na Makazi ambalo linalenga kujua idadi ya watu na kutoa huduma kulingana na mahitaji”

Aliongeza kuwa Serikali  itachukua hatua kwa wale wote watakaopotosha kuhusu zoezi la Anwani za Makazi  kwa kutoa taarifa zisizo na ukweli kwa wananchi ikiwemo kuwaeleza kuwa namba hizo katika majengo yao zitatumika kuwatoza kodi.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Kundo ameitaka Wakala wa  Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanatekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa  mwezi Machi mwaka huu yakuitaka TARURA kuweka  nguzo katika barabara zote wanazozisimamia.

“Taasisi zote za Umma na Binafsi, zishiriki kujiwekea miundombinu ya Mfumo katika maeneo ya ofisi zao ama maeneo yao ya uwekezaji kote nchini. Vilevile, kwa Upande TARURA na TANROAD wameelekezwa kusimika nguzo zenye majina ya barabara au mitaa wanayoihudumia” Alisisitiza Naibu Waziri Kundo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi