Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uhuru wa Mtandao Utumike Kulinda Utamaduni
Sep 28, 2023
Uhuru wa Mtandao Utumike Kulinda Utamaduni
Waziri wa Habari, Mawasilino na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye akizungumza leo Alhamisi Septemba 28 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa la uhuru wa mitandao barani Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam
Na Chedaiwe Msuya

Waziri wa Habari, Mawasilino na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye  amesema nchi itaendelea kuwa muumini wa uhuru wa mtandaoni huku akitoa rai kuwa uhuru huo unapaswa utumike kulinda tamaduni za Bara la Afrika.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 28 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa la uhuru wa mitandao barani Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam  na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka nchi mbalimbali.

Waziri Nape amesema  nchi kutoa uhuru ni jambo zuri hivyo wananchi wanapaswa kulinda tamaduni kwa kutumia mitandao hiyo katika shughuli za kuwaingizia kipato na si kutumia katika mambo ambayo yanaweza kuvunja amani ya nchi.

"Tumeweka katika sera zetu uhuru wa mitandao lakini sasa hivi dunia imekuwa digitali, tumieni mitandao hiyo kufanya shughuli za kiuchumi na si kufanya mambo ambayo hayasaidii chochote na mitandao ni fursa, "amesema Nape.

Amesema pamoja na kuwa na uhuru mtandaoni nchi za Afrika zinapaswa kulinda utamaduni wake na ili kuepusha nchi hizo kuingia kwenye matatizo ambayo yatapelekea kuharaibu amani na kuleta machafuko.

"Tusiondoke kwenye mtandao kila mtu ajiunge huko lakini tuhakikishe tunabaki salama kwa maslahi ya nchi zetu na kubadilisha maisha yetu kwa kufanyabiashara," amesema.

Waziri Nape amesema kuwa nchi inajipanga siku zijazo iweze kutumia teknolojia kwenye uchaguzi ili kumwezesha kila mtu kuchagua viongozi popote atakapokua.

"Tunataka ifike mahali kila mwananchi awe na uwezo wa kupiga kura mtandaoni kusiwe na haja ya kwenda kwenye vituo na kupanga foleni kama kila mtu anaweza kutumia simu basi inawezekana ni sisi kuamua kwa kuweka sera nzuri na utekelezaji"ameongeza Nape

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira amesema kuwepo kwa mkutano huo nchini kumetokana  na juhudi zinazofanywa na Rais Dk  Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kimataifa na kuimarisha uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi