Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tulilinde Ziwa Victoria ili litupe Matunda-Byabato
Sep 26, 2023
Tulilinde Ziwa Victoria ili litupe Matunda-Byabato
aibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Afrika Mashariki), Mhe. Steven Byabato leo Septemba 26, 2023 akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati alipofika mkoani humo kwa ajili ya ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Kisekta mkoani humo.
Na Paulo Zahoro, Mwanza

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Afrika Mashariki), Mhe. Steven Byabato leo Septemba 26, 2023 amefika Kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufuatia ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Kisekta mkoani humo.

Akiongoza ujumbe wake kwenye mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Byabato ametoa wito kwa wadau kwenye ukanda huo kulilinda Ziwa Victoria kwa maslahi ya vizazi vya sasa na baadae.

Amesema ziwa hilo linalounganisha mataifa mbalimbali Afrika kwa dahari ya miaka limekua likistawisha uchumi wa Utalii na ukuaji wa Sekta ya Uvuvi hususani kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo kila mmoja anapaswa kulilinda lisiharibiwe wala kuchafulia.

Tunalilinda ziwa letu ili nalo litulinde sisi, sheria za usimamizi wa bonde la Ziwa Victoria ni lazima zizingatiwe ili ziwa letu lilete matunda kwetu sio tu kwa usafirishaji na chakula bali hata kwa uchumi wa uvuvi na Utalii, “ amesema Mhe. Byabato.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati mkoani humo huku akitolea mfano wa Daraja la Kigongo Busisi, Meli ya MV Mwanza, Machinjio ya Kisasa, Miradi ya Usafi wa Mazingira pamoja na Mradi wa Maji wa Butimba ambao uko mbioni kukamilika.

Mhe. Makilagi amefafanua kuwa miradi hiyo ni kielelezo kwamba Mhe. Rais Samia amekusudia kuwahudumia wananchi kwa kuwaondolea kero kwenye huduma za kijamii kwenye sekta za Miundombinu, Maji, Afya, Kilimo, Usafi wa Mazingira na Elimu.

Ziara ya Mhe. Byabato mkoani Mwanza imejikita kwenye ukaguzi wa miradi mbalimbali ukiwemo Mradi wa Usafi wa Mazingira Pasiansi unaosimamiwa na Bonde la Ziwa Victoria ambapo atajionea hatua ya utekelezaji iliyofikiwa kwenye miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi