Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yakubali Kuiuzia India Mbaazi Kuanzia Sasa hadi Machi 2025
Feb 24, 2024
Tanzania Yakubali Kuiuzia India Mbaazi Kuanzia Sasa hadi Machi 2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Waziri wa Biashara na Viwanda wa India, Mhe. Piyush Goyal walipokutana kwa mazungumzo jijini New Delhi.
Na Mwandishi Wetu

Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 24 Februari, 2024 wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Mwenyeji wake Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchini humo, Mhe. Piyush Goyal yaliyofanyika jijini New Delhi. 

 

Kadhalika, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana Tume ya Pamoja ya Biashara kukutana mwezi Aprili 2024 ili kuweka mikakati ya pamoja ya kukuza biashara baina ya Tanzania na India. 

 

Awali kabla ya kufikiwa kwa makubaliano haya, Tanzania iliruhusiwa kuuza kiasi cha tani laki mbili pekee za mbaazi kwa mwaka  nchini India. 

 

Waziri Makamba alikuwa nchini India kushiriki Mkutano wa Rais na 2024 sambamba na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini humo mwezi Oktoba 2023.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi