Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania, Kongo Kuandaa Mkutano wa Wafanyabiashara
Feb 26, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema  Tanzania na Kongo zimepanga  kuandaa mkutano mkubwa wa pamoja kati ya wafanyabiashara wa nchi hizo ili kuzungumzia mwelekeo wa kibiashara.

Amesema kuwa mkutano huo ambao utajadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara wa nchi mbili hizo na namna ya kuzitatua utasaidi kuchochea uchumi wa kitaifa na wa mtu mmoja mmoja.

Amesema hayo jana (Februari 25, 2022) baada ya mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),  Sama Lukonde yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu huyo jijini  Kinshasa.

“Tuna fursa katika ziwa Tanganyika ambapo Tanzania tumejenga bandari tano muhimu zinaoweza kutumiwa na DRC, pia tuna barabara tunayoitumia  kutoka Tunduma kwenda Kaprimposhi-Kasumbalesa,  tunataka kubadilisha “route” ipite kwenye daraja la Kasenga barabara ambayo ni fupi sana inapunguza zaidi ya kilomita 2000 kwenda na kurudi.

Mhe. Majaliwa amesema wamekubaliana kutembeleana ili kuimarisha utendaji na ufutiliaji pamoja na kuimarisha uhusiano.

Awali, Waziri Mkuu alikutana na watumishi katika ubalozi wa Tanzania nchini DRC na aliwataka kuongeza ubunifu ili kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi hiyo na Tanzania.

“Tunapozungumzia Ubalozi maana yake  tunawataka  muimarishe diplomasia yetu , ongezeni  ubunifu ili tuweze kunufaika na mahusiano haya”

Mhe. Majaliwa amerejea nchini baada ya kumalizika  kwa Mkutano wa Kumi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Mpango wa Amani,   Usalama na Ushirikiano na DRC pamoja na  Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika jijini Kinshasa,  ambapo alimwakilisha Rais  Samia Suluhu Hassan.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi