[caption id="attachment_3355" align="aligncenter" width="630"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akifungua Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Wanaomsikiliza ni wadau kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.[/caption]
Na Mwandishi Wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) zimeanza kutoa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za ukopeshaji katika kilimo.
[caption id="attachment_3359" align="aligncenter" width="630"]Mafunzo hayo ya siku sita yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma hasa kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kuweza kutoa huduma kwa wakulima kwa wakati na kuzingatia tija kwa wakulima nchini ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo.
Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa TADB alisema kuwa katika kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini Tanzania, TADB imeamua kuwajengea uwezo wadau kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kwa kushirikiana na NABAD na MIVARF ili kuweza kutoa huduma kwa uhakika ili kuwakomboa wakulima nchini.
[caption id="attachment_3365" align="aligncenter" width="630"]