Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Simbachawene awataka Ma DC na Wakurugenzi Kuzingatia Mipaka yao ya Kazi
Jul 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6214" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika ukumbi waHazina Ndogo mjini Dodoma. (Picha na: OR - TAMISEMI)[/caption]

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene,  amewataka  Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini,  kuzingatia mipaka yao ya kazi ili kuepusha migongano ya mara kwa mara pamoja na   kushirikiana kwa pamoja ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo mjini Dodoma leo katika ukumbi wa hazina ndogo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI  kwa kushirikiana na  Taasisi ya Uongozi kwaajili ya kuwajengea uwezo  Wakurugenzi pamoja na Wakuu wa  Wilaya kutoka katika mikoa mitano ya Mara, Simiyu, Mwanza, Geita pamoja na Manyara.

“Sisi Viongozi ni kama timu ya mpira, hivyo ni lazima kila mmoja katika namba yake acheze ipasavyo ili kuleta ushindi, lakini pia  pasiwepo na mtu ambaye atacheza kwa kuingilia nafasi ya mwenzie maana kwa kufanya hivyo lazima kutatokea mgongano katika utendaji kazi” Alisema.

[caption id="attachment_6223" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akiwasili katika ukumbi wa Hazina Hdogo mjini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi. Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tano.[/caption]

Vilevile Mheshimiwa Simbachawene  amewataka viongozi hao kwa kupitia mafunzo hayo kwenda kufanya mabadiliko ya kiutendaji  kwa kuwa wabunifu ili kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao wenyewe kwa wenyewe  ili kutimiza lengo la pamoja la kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya hayo Kaimu  Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo alizitaja mada ambazo zitatolewa kwa viongozi hao kuwa ni Mbinu za Uongozi, Majukumu na Mipaka ya  Kazi, Muundo wa Serikali na namna Serikali inavyofanya kazi, Utunzaji wa Siri za Serikali pamja na Maadili katika Utumishi wa Umma.

[caption id="attachment_6224" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo yaWakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.[/caption]

Mafunzo hayo kwa  Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni muendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa viongozi  na Wakurugenzi hao Tanzania Bara ambayo yanafanyika

kwa awamu ambapo hatimaye  yatakuwa yamefanyika kwa Wakuu wa Wilaya zote Tanzania Bara.

Ufunguzi huo pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Musa Iyombe pamoja na Wakurugenzi mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi