Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shilingi Bilioni 40 Zatatua Changamoto za Wananchi Kongwa
Nov 01, 2023
Shilingi Bilioni 40 Zatatua Changamoto za Wananchi Kongwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo akizungumza mbele Waandishi wa Habari leo jjijini Dodoma, katika kampeni ya ‘ Tumekusikia Tumekufikia’ inayoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) ambayo inawakutanisha Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Watendaji wa Halmashauri kuongea na waandishi wa habari
Na Jonas Kamaleki - Dodoma

Serikali imezisikia changamoto za wananchi wa Kongwa na imewafikia kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 40 katika kipindi cha miaka mitatu katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Katika Sekta ya Elimu, shilingi bilioni 12.24 zimetolewa kwa kujenga madarasa 449 (160 shule za msingi na 289 shule za sekondari), nyumba za walimu 9, maabara 29, mabweni 16, majengo ya utawala 4, maktaba 2 katika shule za sekondari.

Akizungumza mbele Waandishi wa Habari leo jjijini Dodom, katika kampeni ya ‘ Tumewasikia Tumewafikia’ inayoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) ambayo inawakutanisha Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Watendaji wa Halmashauri kuongea na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo amesema zimejengwa shule mpya 7 za msingi na 13 za sekondari na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani pamoja na utoro.

Dkt. Nkullo ameongeza kuwa shilingi bilioni 8.14 zimetolewa kwenye Sekta ya Afya ambapo zimejenga majengo mapya 10 ya hospitali ya wilaya, vifaa tiba, ujenzi wa Vituo vya Afya vipya vitano na Zahanati nane.

Kwenye eneo ya kuwezesha wananchi kiuchumi Serikali imeyawezesha makundi maalum ya wanawake, wenye ulemavu na vijana kwa kuwapa mikopo bila riba kutoka kwenye asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri, ndani ya miaka mitatu Halmashauri hiyo imetoa shilingi milioni 711, 844,900 kwa wanufaika 890.

Kwenye kilimo Serikali imetoa shilingi milioni 690 zilizotumika kujenga miundombinu ya umwagiliaji 

“Serikali inajenga Kituo Mahiri cha Mafunzo na Usimamizi wa Mazao baada ya Mavuno kwa ajili ya kudhibiti sumu kuvu kwa gharama ya shilingi bilioni. 18.3, ujenzi umefika zaidi ya 60%,” amesema Dkt. Nkullo.

Dkt. Nkullo aliongeza kuwa Serikali imetoa shilingi milioni. 322 kwa kujenga majosho 14 kwa ajili ya kuogesha na kutibu mifugo, hili ni ongezeko la majosho kutoka majosho 8 hadi 22.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi