Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali za Tanzania na Kenya Zamaliza Mzozo wa Vikwazo Vya Biashara Baina ya Mataifa Hayo.
Sep 09, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_12800" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.[/caption]  

Na: Ismail Ngayonga

SERIKALI za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka baina ya nchi hizo mbili  hatua inayokusudia  kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda  mara baaada ya kumalizika kwa mkutano wa  pamoja yao ulioshirikisha Viongozi Waandamizi wa  Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa hayo.

[caption id="attachment_12801" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana akitoa taarifa ya majadiliano ya mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Kenya uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.[/caption] [caption id="attachment_12802" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Baishara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.[/caption]

Anasema katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.

Prof. Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo,  Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.

[caption id="attachment_12803" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.[/caption] [caption id="attachment_12804" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo na Mwenjeji wake Prof. Adolf Mkenda wakionyesha Sera ya Taifa ya Biashara ya Kenya wakati mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam.(Picha na: Eliphace Marwa-Maelezo)[/caption]

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda alisema mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku tatu ulilenga kumaliza changamoto za biashara zinazojitokeza kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, ambapo Timu za Wataalam wa Serikali hizo ambapo hoja hizo zimeweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi wa pamoja, hatua inayolenga kufungua upya milango ya ushiriakiano baina ya Wafanyabiashara na Wakulima wa Tanzania na Kenya.

“Katika majadiliano yetu tumekubaliana kuwa sasa bidhaa ya gesi ya kupikia na ungano wa ngano ambazo zilizuliwa kuingia Kenya sasa zitaruhusiwa kuingia nchini humo, na sisi kwa upande wetu Tanzania tumeruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya zianze kuingia nchini” alisema Prof. Mkenda.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi