Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yapongezwa na Wakazi wa Lindi
Sep 19, 2023
Serikali Yapongezwa na Wakazi wa Lindi
Wakazi wa mkoani Lindi wakiwa katika jukwaa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifanya ziara mkoani humo.
Na Immaculate Makilika - MAELEZO

Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kupongezwa kwa jitihada zake za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Wakazi wa Wilaya ya Lindi kutoka maeneo mbalimbali wakizungumza leo na Afisa Habari wa Idara ya Habari - MAELEZO wamepongeza utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayofanywa na Serikali katika mkoa wao.

Mkazi wa Tulieni, Bw. Issa Omary  amesema kuwa Mkoa wa Lindi umepata neema ya miradi mbalimbali ambayo wanaamini itaendelea kubadilisha maisha yao.

"Uwepo wa  Hospitali ya Rufaa  hapa kwetu unatusaidia kwa sababu awali tulikua tunatibiwa katika Hospitali ya Sokoine ambayo iko mbali  kutoka hapa", amebainisha Bw. Issa.

Naye, Mkazi wa Kata ya Mwenge, Bi. Neema  Nasoro amesema "Tunaipongeza Serikali kwa kujenga shule hii ya kisasa ya Sekondari ya Wasichana Lindi itasaidia watoto wetu kusoma bila kusafiri umbali mrefu kwenda Shule ya Mitwero, hivyo uwepo wake utasaidia sana  watoto wa kike kutimiza ndoto zao".

Ameongeza "Tumefurahi kwa Serikali kujenga Bandari ya kwanza ya Uvuvi hapa Kilwa ni matumaini yangu itasaidia kukuza shughuli za sekta ya uvuvi nchini".

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi