Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuimarisha Ulinzi na Usalama
Sep 05, 2023
Serikali Kuimarisha Ulinzi na Usalama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea taarifa ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura mara baada ya kuwasili kwenye Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.
Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Serikali iimeendelea kutoa kipaumbele na kujizatiti katika kuimarisha ulinzi na usalama ili wananchi na wafanyabiashara waendelee kutekeleza shughuli zao za maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi.

“Serikali imejizatiti na inaendelea kutoa kipaumbelea katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini kwa maana hii tunaendelea kuwezesha vikosi vyetu mbalimbali ili kufanya nchi yetu kuwa salama na tulivu. Ndio maana tunaendelea kuliwezesha Jeshi la Polisi ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa,” amesema Rais Samia.

Ameongeza, “niwaombe sana muimarishe dhana ya ulinzi shirikishi, dhana hii ijengeke na kuimarika ili kila mmoja alipo ahakikishe kwamba usalama wa mahali alipo unamtegemea yeye”.

Kuhusu kuimarisha mazingira ya kazi na makazi ikiwa ni pamoja na kuongeza zana na vitendea kazi, kuhamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na mafunzo kwa askari, Mhe. Rais Samia amesema kuwa Tume ya Haki Jinai iliwasilisha mapendekezo yake juu ya changamoto zilizobainika kwa taasisi, ambapo kuna changamoto zinazozikabili taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi na  aliahidi kuwa Serikali itazifanyia kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Kamilius Wambura amesema kuwa hali ya nchi ipo salama, shwari na tulivu inayowawezesha wananchi kuendelea na majukumu yao ya kukuza uchumi wa taifa. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha usalama barabarani na kuweka mikakati mahsusi ya kuzuia ajali za barabarani ambazo zimekuwa na athari kubwa kwa wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi