Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Hatua kwa Hatua Hadi Stendi, Nyumba za Wageni Kutoa Elimu ya Ebola
Oct 10, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na. Faustine Gimu - Bukoba Kagera.

Katika kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini baada ya hivi karibuni kuripotiwa visa vya ugonjwa huo nchini Uganda, Serikali kupitia wizara ya Afya kwa kushirikiana na watalaam mbalimbali wa afya ngazi ya mitaa hadi taifa wameendelea kutoa elimu hiyo ambapo Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera, Dkt. Issessanda Kaniki ametembelea mitaa mbalimbali  mjini Bukoba ikiwemo  kituo cha mabasi Bukoba pamoja na nyumba za kulala wageni (Guest) kutoa elimu hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  leo Oktoba 10,2022 mara baada ya kufika kituo cha mabasi Bukoba, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt. Issessanda Kaniki amesema hiyo ni katika mwendelezo wa kujipanga katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kuzingatia kanuni na masharti ya afya.

Tumeendelea kuelimisha wananchi hasa abiria katika tishio hili la ugonjwa wa Ebola pia tumeendelea kukagua miundombinu, usafi na uhakika wa magari ambayo yanabeba, hivyo tunahamasiha wananchi kuendelea kujikinga ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka ikiwezekana kutumia vitakasa mikono,”amesema.

 “Mwitikia ni mkubwa kwani kupitia kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na watoa huduma ngazi ya jamii nao wamekuwa wakipita nyumba hadi nyumba kuhakikisha elimu ya Ebola inafika kwa kila mtu,”amemalizia Dkt. Kaniki.

Nao baadhi ya wananchi wakiwemo makondakta na madereva katika kituo cha mabasi Bukoba wamesema hatua ya Serikali kuweka kipaumbele utoaji wa elimu ya Ebola kabla ya madhara kutokea ina umuhimu mkubwa katika kunusuru afya kwa jamii.

Pamoja na kwamba Tanzania hatujapata Ebola, nawasihi Watanzania tuendelee kutii maelekezo ya serikali kwani ina nia njema ya kutulinda tufuate kanuni za afya,”amesema Shakilu Adam

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Moses Machali amesema wao kama wilaya wamejipanga kuwa na vifaa tiba vya kutosha ambapo pia kuna eneo maalum limetengwa kwa ajili ya matibabu iwapo kuna mtu atabainika kuwa na maambukizi ya Ebola.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amesema wilaya imejipanga kuzuia Ebola katika matukio mbalimbali yanayokutanisha watu ikiwemo tukio la uzimaji wa mwenge kitaifa Oktoba 14, 2022. Ikumbukwe kuwa tangu visa vya Ebola viripotiwe nchini Uganda, Tanzania bado ipo salama na imekuwa mstari wa mbele kwa kuchukua tahadhari mapema katika kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama na wanaendelea na majukumu yao ya kila siku ambapo timu za watalaam kutoka wizara ya afya wameweka kambi katika mikoa ya mipakani  na yenye hatari ya

Aidha,Mkuu huyo wa wilaya amesema  wilaya imejipanga kuzuia Ebola katika matukio mbalimbali yanayokutanisha watu ikiwemo tukio la uzimaji wa mwenge kitaifa Oktoba 14,2022.

Ikumbukwe kuwa tangu visa vya Ebola viripotiwe nchini Uganda,Tanzania bado ipo salama ila imekuwa mstari wa mbele kwa kuchukua tahadhari mapema katika kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama na wanaendelea na majukumu yao ya kila siku ambapo timu za watalaam kutoka wizara ya afya wameweka kambi katika mikoa  ya mipakani  na yenye hatari ya kupata maambukizi mapema kutokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali ikiwemo  Kagera.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi