Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ruangwa Wajivunia Rais Samia
Sep 18, 2023
Ruangwa Wajivunia Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi (hawapo pichani) wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani humo leo.
Na Immaculate Makilika - MAELEZO

Wananchi  wa Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi wameonesha kupongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujio wake katika wilaya hiyo umewapa faraja.

Wakazi hao wakizungumza katika nyakati tofauti leo wilayani hapo wamesema kuwa, Serikali imeboresha maisha yao kwa kuwafikishia huduma mbalimbali.

Mkazi wa Kilimahewa Wilaya ya Ruangwa, Bi. Rahma Hokororo amesema kuwa ziara ya Rais Samia katika  Wilaya ya Ruangwa inawapa matumaini kuwa miradi mingi zaidi ya  maendeleo itatekelezwa kwa manufaa yao.

Pia, amemshauri Mhe. Rais Samia kuendelea kufanya kazi, kwani wao wanaunga mkono jitihada zake za kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezwa nchini.

"Tunayaona  maendeleo kwa macho sio kusimuliwa, kwa kweli ana jitihada sana katika kutusaidia Watanzania. Kama mwanamke  ameonesha  jitihada kubwa sana, siku za nyuma tuliambiwa  wanawake hatuwezi chochote lakini yeye ameonesha  wanawake tunaweza, Watanzania tuendelee kumuamini Mhe. Rais",  amesema Bi. Rahma.

Mkazi wa Mtaa wa Likangala na Mjasiriamali, Bi. Zainab Ajibu,  amesema kuwa  Ruangwa kuna umeme wa uhakika na barabara zinaendelea kujengwa hivyo wananchi hao wanapongeza jitihada hizo za Serikali.

"Mfano kuna maji, umeme na mradi wa madini unatekelezwa katika vijiji vya Namikulo, Mihewe na Matambalale, mradi huu unasaidia vijana kupata ajira za muda mfupi na lakini na kupata fedha za kuhudumia familia zao", amebainisha Bi. Ajibu.

Aidha, amesema kuwa huduma za afya ikiwemo za uzazi zimeendelea kuimarika na kupatikana  kwa urahisi na haraka  wilayani humo.

Pia, Bw. Abubakar Mkwepu amesema kuwa waanamini ujio wa Mhe. Rais  utawapa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajasiriamali kuuza bidhaa zao na wengine kuona fursa za uwekezaji zilizopo wilayani humo.

"Baadhi ya miradi imekamikika, mfano Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, pia kuna vituo vya afya ikiwemo  cha Mbuyuni vimekamilika na tayari vimeanza kutoa huduma kwa kweli tunampongeza na kumshukuru Rais Samia", ameeleza Bw. Mkwepu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi