Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Atoa Vifaa vya Michezo kwa Timu Zote za Kombe la Yamleyamle
Jul 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na John Mapepele


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye  kuwapata wachezaji bora na wenye  vipaji ambao wataunganishwa  kwenye timu ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira 45 kwa ajili ya timu hizo na jezi.

“Niwaombe  tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON,  tuleteeni orodha  ya  vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye timu zetu za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi  ya Serikali zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa.

Amewapongeza kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaandaa mashindano ya AFCON 2027 na kusisitiza kuwa inawezekana iwapo kila mdau atachukua wajibu wake.

Aidha, amefafanua kuwa eneo la soka ndilo eneo pekee ambalo  linaweza  kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi ya dini zao, rangi wala  makabila yao.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi