Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Azindua Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar
Mar 20, 2024
Rais Dkt. Mwinyi Azindua Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Shaban Ali Othman na (kushoto kwake) ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Kepteni Hamad Bakar Hamad, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kwa ajili ya Uzinduzi wa Duru ya Kwanza ya utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia kwa Wawekezaji, iliyofanyika leo 20-3-2024.
Na Ikulu - Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizindua Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar leo 20-3-2024.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Shaban Ali Othman akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuzindua Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia kwa Wawekezaji, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-3-2024.
Viongozi wa Serikali wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuzindua Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia kwa Wawekezaji Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 20-4-2024.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi