Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Awasili Zambia Kushiriki Mkutano wa SADC
Mar 22, 2024
Makamu wa Rais Awasili Zambia Kushiriki Mkutano wa SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia tarehe 22 Machi, 2024. Makamu wa Rais anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika) pamoja na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC).
Na Ofisi ya Makamu wa Rais

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi