Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nataka Tujitegemee Kwenye Mbegu Ifikapo 2025 – Rais Samia
Sep 07, 2023
Nataka Tujitegemee Kwenye Mbegu Ifikapo 2025 – Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tarehe 07 Septemba, 2023.
Na Georgina Misama – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeviboresha vituo  vya utafiti na mashamba ya uzalishaji mbegu kutokana na kujiingiza kwenye masuala ya uzalishaji mbegu za kisasa (high breed) na kwamba lengo ni nchi kuweza kujitegemea kwenye mahitaji ya mbegu.

Akizungumza katika Mkutano Maalumu na Vijana, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika Jijini Dar es saalam leo Septemba 07, 2023 Mhe. Rais Samia amesema Serikali imewekeza kwenye masuala ya utafiti pamoja na matumizi ya Mifumo ya Mawasiliano (ICT) ikiwa ili kukuza uzalishaji wa mbegu na nafaka.

“Tunataka ifikapo 2025 robo tatu ya mbegu zote zinazotumika hapa nchini zizalishwe hapa kama sio kujitegemea kabisa. Tunataka mbegu zilizothibitishwa na zinazoendana na aina ya udongo wetu pamoja na kustahilimi mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Rais, Mhe. Samia.

Akijibu swali la Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni ya Eat Fresh Bi Khadija Jabir aliyetaka kujua hatua za Serikali katika kutafuta masoko na kuongeza thamani kwa mazao yanayozalishwa na vijana nchini, Rais Samia alisema Serikali imefanya ufatiliaji na tathimini katika mnyororo mzima wa kuzalisha mpaka kuuza kwa mazao mbalimbali na kuchukua hatua ambazo zimeanza kutoa matokeo chanya.

“Tunawaunganisha wakulima na masoko kwa kutumia vyama vya ushirika, bado hatujafanya vizuri lakini kwa mazao tuliyoanza nayo kama Korosho na Mbaazi yanafanya vizuri. Mwaka jana bei ya mbaazi ilikuwa Shilingi 300 kwa kilo moja, mwaka huu bei ikapanda mpaka Shilingi 2,000 kwa kilo moja, tunataka twende na utaratibu wa vyama vya ushirika kwa mazao yote ili wanunuzi washindane kwenye bei na mkulima auze kwa bei yenye faida,” alisema Rais Samia.

Vilevile Serikali inafatilia kujua mahitaji ya mazao kabla ya kuzalisha ambapo inaiwezesha kujua aina ya zao na masoko upatikanaji wa masoko, aidha, inaimarisha miundombinu ya usafirishaji  wa mazao hayo wa Sekta zote ikiwemo usafiri wa anga, nchi kavu na majini kama vile ujenzi wa barabara, ununuzi wa Ndege ya mizigo, ujenzi wa sehemu maalum ya kuhifadhia mazao yanayohariba haraka bandarini yakisubiri kusafirishwa (Green belt) na ujenzi wa reli ya kisasa.
 
Akitolea maelezo suala la matumizi ya ICT, Mhe. Rais Samia alisema wakulima wanasajiliwa na kupatiwa huduma kwenye mifumo, aidha, Maafisa ugani wamewezeshwa kwa vifaa maalumu vinavyowawezesha kuchukua taarifa hususan za afya ya udogo na umwagiliaji vilevile Serikali imewekeza kwenye matumizi ya mashine za kisasa hasa kwenye mradi wa Building Better Tomorrow (BBT)  kama chachu kwa vijana.

Baadhi ya Viongozi Wakuu wa Nchi mbalimbali Afrika, Wakuu wa Taasisi, Viongozi Wastaafu, Wadau wa Kilimo pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tarehe 07 Septemba, 2023.

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeviboresha vituo  vya utafiti na mashamba ya uzalishaji mbegu kutokana na kujiingiza kwenye masuala ya uzalishaji mbegu za kisasa (high breed) na kwamba lengo ni nchi kuweza kujitegemea kwenye mahitaji ya mbegu.

Akizungumza katika Mkutano Maalumu na Vijana, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika Jijini Dar es saalam leo Septemba 07, 2023 Mhe. Rais Samia amesema Serikali imewekeza kwenye masuala ya utafiti pamoja na matumizi ya Mifumo ya Mawasiliano (ICT) ikiwa ili kukuza uzalishaji wa mbegu na nafaka.

“Tunataka ifikapo 2025 robo tatu ya mbegu zote zinazotumika hapa nchini zizalishwe hapa kama sio kujitegemea kabisa. Tunataka mbegu zilizothibitishwa na zinazoendana na aina ya udongo wetu pamoja na kustahilimi mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Rais, Mhe. Samia.

Akijibu swali la Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni ya Eat Fresh Bi Khadija Jabir aliyetaka kujua hatua za Serikali katika kutafuta masoko na kuongeza thamani kwa mazao yanayozalishwa na vijana nchini, Rais Samia alisema Serikali imefanya ufatiliaji na tathimini katika mnyororo mzima wa kuzalisha mpaka kuuza kwa mazao mbalimbali na kuchukua hatua ambazo zimeanza kutoa matokeo chanya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, Rais wa Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye, Rais wa Senegal, Mhe. Macky Sall, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tarehe 07 Septemba, 2023.

“Tunawaunganisha wakulima na masoko kwa kutumia vyama vya ushirika, bado hatujafanya vizuri lakini kwa mazao tuliyoanza nayo kama Korosho na Mbaazi yanafanya vizuri. Mwaka jana bei ya mbaazi ilikuwa Shilingi 300 kwa kilo moja, mwaka huu bei ikapanda mpaka Shilingi 2,000 kwa kilo moja, tunataka twende na utaratibu wa vyama vya ushirika kwa mazao yote ili wanunuzi washindane kwenye bei na mkulima auze kwa bei yenye faida,” alisema Rais Samia.

Vilevile Serikali inafatilia kujua mahitaji ya mazao kabla ya kuzalisha ambapo inaiwezesha kujua aina ya zao na masoko upatikanaji wa masoko, aidha, inaimarisha miundombinu ya usafirishaji  wa mazao hayo wa Sekta zote ikiwemo usafiri wa anga, nchi kavu na majini kama vile ujenzi wa barabara, ununuzi wa Ndege ya mizigo, ujenzi wa sehemu maalum ya kuhifadhia mazao yanayohariba haraka bandarini yakisubiri kusafirishwa (Green belt) na ujenzi wa reli ya kisasa.
 
Akitolea maelezo suala la matumizi ya ICT, Mhe. Rais Samia alisema wakulima wanasajiliwa na kupatiwa huduma kwenye mifumo, aidha, Maafisa ugani wamewezeshwa kwa vifaa maalumu vinavyowawezesha kuchukua taarifa hususan za afya ya udogo na umwagiliaji vilevile Serikali imewekeza kwenye matumizi ya mashine za kisasa hasa kwenye mradi wa Building Better Tomorrow (BBT)  kama chachu kwa vijana.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi