Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Sangu Awafunda Wanajopo wa Kada ya Afya, Asisitiza Uadilifu
Sep 11, 2024
Naibu Waziri Sangu Awafunda Wanajopo wa Kada ya Afya, Asisitiza Uadilifu
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na wataalamu kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Na Lusungu Helela- Arusha

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amewataka wanajopo la usaili kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanatenda haki huku akisititiza ajira ni suala la usalama wa nchi.

 

Ametoa kauli hiyo leo jijini Arusha wakati akizungumza na wataalamu kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

 

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha haki inatendeka kwa kila msailiwa ili atakayeshinda ashinde kwa haki na atakayeshindwa ashindwe kwa haki.

 

Mhe. Sangu ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanajopo hao kutanguliza mbele maslahi ya taifa huku akionya yeyote atakayethubutu kuvuruga zoezi hilo atakuwa ameingia kwenye matatizo makubwa

 

‘’Tunatafuta vijana watakaoingia Serikalini katika Utumishi wa Umma si chini ya miaka 25 na wengine wenye umri mdogo mpaka miaka 30 kwahiyo, tukifanya makosa tukapeleka vijana wasio na sifa, uadilifu na mengineyo tutaligharimu taifa kwa zaidi ya miaka 25

 

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Sangu amewataka wasaili hao kujiepusha na tabia ya kupendelea na pale inapotokea jambo la kujadiliana lijikite katika kutenda haki.

 

"Tunataka haki itendeke na ionekane imetendeka kwa wasailiwa wote " amesisitiza Mhe. Sangu.

 

Amesema kwa mujibu wa sera ya ajira toleo la pili la mwaka  2008 inaelekeza kuwa ajira zote zipatikane kwa ushindani .

 

“Maombi yamekuwa mengi sana, kati ya nafasi 12,000 zilizotangazwa za kada ya afya, zaidi ya vijana 47,000 wameomba. Kwenye ualimu jumla ya vijana walioomba ni 200,000 kati nafasi za ajira za ualimu 11,015 zilizotangazwa hivyo hakuna njia nyingine ya kupata watumishi pasipo kushindanisha.” Amesema Mhe. Sangu.

 

Amesema kwa sasa vijana wengi wamemaliza vyuo na wapo mtaani ila kutokana na bajeti ya serikali na hali ya uchumi haiwezi kuwa na bajeti ya kuajiri vijana wote waliomaliza vyuo

 

Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan ambapo katika kipindi chake cha miaka mitatu ametoa vibali vya ajira zaidi ya 100,000 ambayo ni idadi kubwa katika kipindi cha miaka mitatu ukifananisha na miaka mitano iliyopita

 

 

Naye Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samuel Tanguye amesema zoezi hili limeshirikisha watalaamu mbalimbali lengo ni kuhakikisha vijana watakaopatika katika machakato huo ni wenye weledi wataokwenda kulisaidia taifa

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi