Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Katambi Afungua Kikao cha Kujadili Matokeo ya Utafiti Kuhusu Athari za UVIKO 19 Katika Shughuli za Kiuchumi za Vijana
Apr 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na: Mwandishi Wetu – Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi leo Aprili 14, 2022 amefungua kikao cha wadau kilichoandaliwa na Shirika la USAID kwa ajili ya kujadili matokeo ya utafiti uliofanyika kuhusu athari za UVIKO – 19 katika shughuli za kiuchumi za vijana.

Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao ambao ulishirikisha wadau mbalimbali zikiwemo Wizara zinazo husika na masuala ya vijana Tanzania bara na Visiwani, Wizara ya Kilimo, viongozi wa Serikali kutoka Mkoa wa Iringa na Mbeya pamoja na Shirika la Feed the Future Tanzania.

Naibu Waziri Katambi katika mkutano huo alielezea mikakati ambayo Tanzania imejiwekea katika kuendelea kutoa fursa mbalimbali kwa vijana zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo alipongeza juhudi zilizofanyika kupitia mradi “Advancing Youth” ambao umewanufaisha vijana 38,500 na kusaidia kuzalisha ajira 3,650 kwa vijana katika sekta rasmi na isiyo rasmi. 

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutambua mchango unaofanywa na wadau mbalimbali katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini. 

Aidha, maandiko ya matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo. pia vijana walionufaika na mradi wa Inua Vijana “Advancing Youth” waliweza kutoa shuhuda kuhusu manufaa ya mradi huo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi