Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha vitabu vya Ripoti ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji cha Chikundi mara bada ya kuzindua Mpango huo wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Rangwa Pride mkoani Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Mkutano huo umebebwa na kaulimbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi kwa Ustawi wa Jamii”. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Bw. Mohamedi Ismail Ngokono Mwenyekiti wa Kijiji cha Chikundi Ripoti ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijiji cha Chikundi Kata ya Mandawa Wilaya ya Ruangwa wakati wa Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Rangwa Pride mkoani Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mzee Jafari mnaheka cheti cha Ardhi ya Kijiji kinachoonesha eneo lote linalomilikiwa na Kijiji cha Juhudi B Kata ya Chinongwe wakati wa Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Ruangwa Pride mkoani Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Ruangwa Pride mkoani Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Mkutano huo umebebwa na kaulimbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi kwa Ustawi wa Jamii”.
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa