Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkakati wa Kutumia Matamasha Kutangaza Utalii Waanza Kuandaliwa
Sep 26, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii zimeanza kutekeleza maelekezo ya Mawaziri, Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na Mhe. Dkt. Pindi Chana ya kubainisha maeneo na mkakati wa ushirikiano katika Sekta za Utamaduni, Sanaa, Michezo pamoja na Utalii waliyoyatoa Septemba 16, 2022, jijini Dodoma.

Kikao hicho cha ngazi ya wataalamu kutoka Wizara hizo kinafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Septemba 26-28, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zilizopo Mtumba Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Aidha, maelekezo hayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa Wizara hizo ambapo alizitaka kukaa pamoja na kundaa mkakati wa pamoja wa kutumia matamasha kukuza Utalii nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi