Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Ndumbaro Apigia “Debe” Filamu za Tanzania Kimataifa
Oct 27, 2023
Mhe. Ndumbaro Apigia “Debe” Filamu za Tanzania Kimataifa
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Oktoba 27, 2023 jijini Dar es Salaam akizungumza katika hafla ya kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa nchi ya Uturuki
Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 27, 2023 jijini D

ar es Salaam ameungana na Raia wa Uturuki wanaoishi hapa nchini kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa taifa hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, Tanzania itendelea kushirikiana na nchi hiyo katika maeneo mbalimbali hususani kuendeleza Sanaa ya Tanzania hasa filamu ili ziweze kufika kiwango cha juu. 



Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Mabalozi pamoja na viongozi wengine wa kidiplomasia.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi