Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio katika Picha: Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Dodoma
Mar 08, 2024
Matukio katika Picha: Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma akiwapungia mkono waandamanaji (hawapo pichani) wakati wakipita mbele ya jukwaa kuu kujitambulisha.
Na Joseph Mahumi

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo (mbele) akiwaongoza baadhi ya watumishi wanawake wa wizara hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, waliojitokeza katika maandamano kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma. 
 
Baadhi ya watumishi Wanawake wa Wizara ya Fedha wakishangilia katikati ya viwanja vya Chinangali II jijini Dodoma eneo ambalo maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanafanyika Kitaifa,mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.
 
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani)  katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Chinangali II wilayani Chamwino mkoani Dodoma

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi