Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Marekani Yaongoza Kuleta Watalii kwa Mwezi Mei
Jul 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Lilian Lundo – MAELEZO


Marekani imeongoza kuleta watalii wengi wanaokuja Tanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kutoka nje la bara la Afrika kwa kipindi cha mwezi Mei mwaka huu.


Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Daniel Masolwa alipokuwa akitoa taarifa ya watalii walioingia nchini kwa kipindi cha Januari mpaka Mei, 2022, leo Julai 14, 2022 katika Ofisi za Takwimu, Jijini Dar es Salaam.


 “Kwa mwezi Mei mwaka huu jumla ya watalii 5,606 waliingia nchini wakitokea nchini  Marekani, wakifuatiwa na  Ufaransa  (4,456), India (4,211), Uingereza(3,294) na Ujerumani (3,160). Aidha watalii walioingia Mei pekee waliongezeka kufikia  89,271 ikilinganishwa na watalii 42,173 walioingia nchini mwezi Mei 2021, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 117.7,” alisema Masolwa.


Aliendelea kusema kuwa  idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini ni matokeo ya kazi nzuri na iliyotukuka iliyofanywa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani Aprili mwaka huu na baadae kuzinduliwa hapa nchini.


“Filamu ya Tanzania the Royal Tour imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Utalii ambapo kwa sasa Tanzania inashuhudia ongezeko kubwa la Watalii. Aidha katika  kipindi cha Januari hadi Mei, 2022 jumla ya watalii 458,048 kutoka nje ya nchi walitembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikilinganishwa na watalii 317,270 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021,” alifafanua  Masolwa

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi