Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mapato Sekta ya Utalii Kufikia Dola Bilioni 16 Mwaka 2025
Oct 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_19171" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho yaTatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption]

Na: Fatma Salum

Sekta ya utalii nchini inakadiriwa kuongeza mapato kufikia dola bilioni 16 ifikapo mwaka 2025 iwapo itawekewa mikakati madhubuti ya kuboresha sekta hiyo ikiwemo miundombinu itakayorahisisha watalii kufika kwenye vivutio.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo leo wakati akifungua Maonesho ya 3 ya Kimataifa ya Utalii (Swahili International Tourism Expo) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

“Kwa mujibu wa ripoti ya 6 ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania imeonesha kuwa ifikapo mwaka 2025 mapato kutokana na sekta ya utalii yataongezeka kufikia dola za kimarekani bilioni 16, hivyo tunajitahidi kuboresha sekta hiyo ili tuweze kufikia makadirio hayo,” alisema Mh.Samia.

[caption id="attachment_19174" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho yaTatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption] [caption id="attachment_19177" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Mstaafu Gaudenci Milanzi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho yaTatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption]

Alieleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi duniani na idadi ya watalii inaendelea kuongezeka ambapo kwa mwaka 2016 ilifika zaidi ya watalii 1,284,279 ambao walifika nchini kujionea vivutio mbalimbali na waliingiza nchini takriban dola bilioni 2.1.

Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa sekta ya utalii katika kukuza uchumi hivyo maonesho hayo ni muhimu kwa wadau wa sekta hiyo kujadili fursa na changamoto zilizopo pamoja na kubadilishana uzoefu ili kuboresha kwenye maeneo yao.

“Tutumie maonesho haya kujitangaza kote duniani ili tuweze kuongeza idadi ya watalii na kukuza uchumi wa Tanzania na bara letu la Afrika kwa ujumla,” alibainisha Makamu wa rais.

[caption id="attachment_19180" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho yaTatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanayoratibiwa na Bodi hiyo. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption] [caption id="attachment_19183" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi. Devotha Mdachi akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption] [caption id="attachment_19189" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu akitembelea baadhi ya mabanda ya washiriki wa maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption] [caption id="attachment_19192" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu akimkabidhi mwakilishi wa Kampuni ya Ethiopia Airline tuzo ya kuthamini mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) katika hafla ya uzinduzi wa maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).[/caption] [caption id="attachment_19195" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_19198" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho yaTatu ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (Swahili International Tourism Expo) leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika Viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Nyerere (JNICC). (Picha na: Frank Shija )[/caption]

Pia alisema kuwa kati ya mwaka 2007 na 2017 utalii wa ndani ya Afrika umekua kutoka asilimia 34 hadi asilimia 44 ya watalii wote wa kiafrika wanaotembelea nchi za ndani ya bara hili.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla aliwapongeza waandaaji wa maonesho hayo wakiongozwa na Bodi ya Utalii Tanzania na kuwataka kutumia fursa hiyo kujitangaza zaidi.

Maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma kutoka nchi za Afrika Kusini, Nigeria, Morocco, Kenya, Uganda, Rwanda na Mauritius.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi