Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa SADC ORGAN TROIKA Nchini Zambia
Mar 23, 2024
Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa SADC ORGAN TROIKA Nchini Zambia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika),Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia. Tarehe 23 Machi 2024.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika), Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia. 

 

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kutambua jukumu la kufanya kazi kwa pamoja ili kumaliza changamoto za kiusalama zinazozikabili Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais Hichilema amesema kutoimarika kwa hali ya usalama na amani katika maeneo hayo kuna athiri Jumuiya katika kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuwa rasilimali zinatumika kurejesha amani katika maeneo hayo. Ametoa wito wa kuendelea kuunganisha nguvu pamoja ikiwemo kushirikisha jumuiya za kimataifa rafiki kama vile Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika), Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia. Tarehe 23 Machi 2024.

Mkutano huo umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi, Rais wa Zimbawe, Mhe. Emmerson Mnangagwa, Rais wa Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa Angola, Mhe. João Lourenço, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi, Makamu wa Rais wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri Mkuu wa Lesotho, Sam Matekane.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi