Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Ashiriki Sherehe za Uapisho Rais Mteule wa Zimbabwe
Sep 04, 2023
Majaliwa Ashiriki Sherehe za Uapisho Rais Mteule wa Zimbabwe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga, wakati alipohudhuria sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Harare, Zimbabwe, Septemba 04, 2023. Mhe. Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe hizo
Na Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Septemba 04, 2023 ameshiriki sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika Uwanja wa Harare, Zimbabwe.

Mhe. Rais Mteule Mnangagwa ameshinda  uchaguzi  huo kwa kura zaidi ya milioni 2.3 kati ya kura milioni 4.4 zilizopigwa sawa na asilimia 52.6 dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa ambaye alipata kura milioni 1.9 sawa na asilimia 44.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Alberto Chissano wakati alipohudhuria sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Harare, Zimbabwe, Septemba 04, 2023. Mhe. Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe hizo

Ushindi huo unamfanya Mhe. Mnangagwa kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.

Mhe. Majaliwa amemuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho huo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi