Majaliwa Akagua Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje wa Jiji la Dodoma
Sep 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli za udongo wakati alipotemblea maabara ya mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 , Septemba 4, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama makaravati wakati alipokagua mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 wakati alipokagua mendeleo ya ujenzi huo, Septemba 4, 2022. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na wa tatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele Mwakibete (wa pili kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3, Septemba 4, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Septemba 4, 2022.