Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Mhandisi Luhemeja Asisitiza Ubunifu kwa Watendaji Wake
Sep 05, 2023
Katibu Mkuu Mhandisi Luhemeja Asisitiza Ubunifu kwa Watendaji Wake
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akikabidhiwa nyaraka kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.
Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka watendaji wa ofisi yake kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa malengo yanayopimika ili kuiwezesha serikali kufikia malengo na kuwahudumia wananchi.

Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo Septemba 5, 2023 mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu ambae amehamishiwa Wizara ya Maji.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza menejimenti ya ofisi hiyo baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, hafla iliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023. 

Ameongeza kuwa, kazi ya kuhudumia wananchi haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu kwa maslahi mapana ya taifa.

Aidha, ameahidi kushirikiana na menejimenti na watumishi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ofisi hiyo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa sita kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu (wa sita kutoka kulia), wakiwa katika picha ya Pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyobaada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Wizarani hapo, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Jamal Katundu ameishukuru Menejimenti na Watumishi kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ambao ulimwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi