Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kasekenya Awataka TEMESA Kuwa Wabunifu
Mar 18, 2024
Kasekenya Awataka TEMESA Kuwa Wabunifu
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mha. Godfrey Kasekenya akifungua Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), leo jijini Dodoma.
Na Neema Macha. TEMESADodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania(TEMESA) kuangalia namna bora ya kuja na ubunifu katika maeneo yao ya kazi ili kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Naibu Waziri ameyasema hayo leo Tarehe 18 Machi, 2024 wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wakala huo ambapo amefanya pia Ufunguzi wa Mkutano wa 15wa Baraza la Wafanyakazi.

Mkutano huo wa Barazala Wafanyakazi umefanyika katika ofisi za TEMESA Makao Makuu mjini Dodoma na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi waliowawakilisha watumishi wenzao kutoka mikoa na vituo pamoja na Mameneja wa Mikoa.

Naibu Waziri Kasekenya amesemawakala unatakiwa kujiendesha kibiashara ili kuongeza pato la serikali na kuwaagiza watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia ushindani wa kibiashara.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Mha. Godfrey Kasekenya,wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi za TEMESA makao makuu,jijini Dodoma.

”Kuweni wabunifuwa vyanzo vipyavya mapato, wabunifukatika matumizi ya mifumo ya TEHAMA na mbinu mbalimbali za kibiashara, ni vyema tukakumbushana kwamba Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi imeweka malengo mbalimbali na utekelezaji wa Ilani hiyo unategemea watumishi wa umma”. Amesema

Kasekenya.

Kasekenya ameongeza kuwa TEMESA inatengeneza magari ya serikali ili kuwawezesha watumishi wenginewa umma kufikia malengo mbalimbali ili kutekeleza majukumuyao, hivyo amewataka wakala kukumbuka dhamana waliyopewa na kuwaasa kusoma na kuelewa na kutekeleza Ilani ya Chama Tawala.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala akitoa neno katika ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika katika Ofisi za TEMESA Makao Makuu,jijini dodoma.

Aidha, kasekenyaamewataka watumishi kuzingatia maadili katika utendejikazi na kutoa rai kwa watumishi wanaofanya biashara na TEMESA kwa kificho au wazi kwa kupitia

kampuni binafsina kupelekea mgonganowa kimaslahi waache tabia hiyo kwa kuwa hawataiwezesha TEMESA kufikia malengo yake waliyojiwekea.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi