Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Yapitisha Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa DCEA na ORPP
Mar 20, 2024
Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Yapitisha Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa DCEA na ORPP
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Na Mwandishi wetu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)  na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP).

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Makadirio hayo yametajwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Florent Laurent Kyombo wakati alipokaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Machi 20, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Laurent Kyombo (akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo) ameongoza kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Bunge kilichopokea Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25

Alisema baada ya majadiliano mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na  Bajeti iliyotengwa,  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeridhia.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis Mutungi akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.

 “Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona Bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” alibainisha.

Kaimu Kamishina Jenerali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Shaaban Mbaraza akiongea jambo katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ameishukuru kamati kwa ushauri na kupitia bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ambayo yatasaidia bajeti hiyo kukaa vizuri wakati kusomwa Bungeni kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi