Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dodoma Yaanza Kutekeleza Programu Utoaji Taarifa za Serikali
Nov 01, 2023
Dodoma Yaanza Kutekeleza Programu Utoaji Taarifa za Serikali
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa progam ya TUMEWASIKIATUMEWAFIKIA inayoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO)
Na Ahmed Sagaff - MAELEZO

Uongozi wa Mkoa wa Dodoma umeanza kutekeleza programu ya Serikali inayolenga kuhakikisha Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi za Majiji, Manispaa na Miji, wanatoa taarifa za utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi.

Akifungua utekelezaji wa mkakati huo leo jijini Dodoma, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema programu hiyo inaratibiwa na Idara ya Habari - MAELEZO.

"Serikali inatoa fedha nyingi kwa maendeleo ya wananchi, matarajio ya Rais Samia kwa Idara ya Habari ni kuongeza chachu ya mawasilianio kati ya Serikali na wananchi, fedha hizi zinatokana na kodi za wananchi, hivyo wanancgi wanapaswa kujua miradi inavyotekelezwa na maendeleo yake," ameeleza Mhe. Nnauye.

Ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuto ushirikiano kwa Idara ya Habari ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa Serikali.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ameeleza kuwa Serikali inatekeleza miradi mingi lakini wananchi hawana taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji.

Dkt. Dugange amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanawatumia Maafisa Habari ktk kutoa taarifa na kuwapatia vitendea kazi ili washiriki kikamilifu katika kutoa taarifa kwa wananchi.

Pamoja na hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amesema uongozi unatambua kero za wananchi na umejitahidi kufikisha huduma za kijamii kwa wananchi licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

Pia, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi ameeleza kuwa  programu hiyo itawezesha kupata shuhuda za wananchi kuhusu miradi inayotekelezwa na Serikali na jinsi inavyowasaidia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi