Dkt. Jingu Aongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi
Sep 27, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu ameongoza kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilicholenga kupokea taarifa ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 pamoja na kujadili Rasimu ya Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi nchini.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa ambaye ni Katibu wa Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi akiwasilisha taarifa ya masuala ya Sensa ya Watu na Makazi wakati wa kikao cha 8 cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 JijiniDar es Salaam.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 27 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Julius Nyerere Interational Covention Centre Jijini Dar es Salaam (JNICC).
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati wa kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 Dar es Salaam.
Jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kuishauri Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa inayoongozwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna bora ya utekelezaji wa masuala ya Sensa.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Zanzibar, Mhe. Balozi Mohamed Haji Hamza akieleza na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya sensa wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wakifuatilia kikao hicho.