Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DARUSO Yampongeza JPM
Jun 16, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_3661" align="aligncenter" width="900"] Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi John Jilili(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kulia ni Makamu wa Rais wa Serikali hiyo bi Anastazia Anthony na kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani Bw. Mabina David.[/caption]

Na Frank Mvungi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kazi za kizalendo anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Mhandisi John Jeremiah amesema wanaunga mkono jinsi suala la mchanga wa madini (makinikia) linavyoshughulikiwa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuleta mageuzi ya kweli na kujenga Tanzania mpya.

“Tofauti na wale wanasiasa wanaobeza juhudi za Rais Mgufuli sisi wana DARUSO tunapenda kumuhakikishia kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi na tunaamini kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi 2017 zitalipwa mara moja”Alisisitiza Jeremiah

[caption id="attachment_3662" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi John Jilili akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani bw. Mabina David.[/caption] [caption id="attachment_3667" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.(Picha na frank Mvungi).[/caption]

Aliongeza kuwa ripoti ya kamati iliyoongozwa na Profesa Michael Ossoro imebainisha kuwa fedha zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu hivyo juhudi za kulinda rasilimali za Taifa zinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania

“DARUSO tunapenda kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mhe. Rais wetu Dkt. Magufuli kwenye mapambano haya.” Alisisitiza Mhandisi Jeremiah.

Mwandisi Jeremiah amesema kuwa kiwango hicho cha fedha kingetosha kuhudumia huduma za kijamii hivyo kuwapa Watanzania unafuu wa maisha.

“Tunapenda kumpongeza Mhe. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za kizalendo zilizomfanya Mwenyekti Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu”.Alisisitiza Mwandisi Jeremiah.

       

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi