Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 27 Kujenga Bwawa la Kilimo cha Umwagiliaji Msagali Mpwapwa
Sep 21, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na. Mwandishi Wetu - Mpwapwa

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo, imekabidhi rasmi kwa Makandarasi GNMS Contractors eneo la Ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha Umwagiliaji litakalojengwa kwa thamani ya Shilingi Bilioni 27.

Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Dodoma, Raphael Laizer amesema wakati wa makabidhiano ya eneo hilo la umwagiliaji jana jioni kuwa, bwawa hilo litakalokuwa na ujazo wa lita milioni tisini, litapelekea kuendelezwa kwa eneo litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta elfu tatu na mia tano (3500), ambapo ujenzi wa bwawa hilo unaotegemewa kuchukua miezi kumi na nane, utahusisha eneo ya unyweshwaji maji mifugo, matumizi ya binadamu na shughuli nyingine za kimaendeleo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kusaidia kundi hili maalum la wakulima, wavuvi na wafugaji na kumuasa mkandarasi na wasimamizi wote wa mradi huu kufanya kazi hii kwa weledi na kwenda na wakati.

Kwa Upande wake Mwananchi kwa kata ya Chunyu, Bi Easther Zeavela alitoa ombi kwa mkuu wa mkoa kuwaasa wasimamizi wa miradi inayokwenda vijijini kuwa makini, kwani mradi mingi inakosa usimamizi mzuri. “Uongozi wa juu unapoleta miradi huku vijijini, wasimamizi wasimamie vizuri ili pesa za miradi zitosheleze, mambo mengi tunaona yanaanzishwa na hayakamiliki.” Alisema mwananchi huyo

Ujenzi wa bwawa la msagali unaelezwa kuleta mafanikio mengi pindi utakapokamilika kutokana na asili ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko ya maramara, hivyo kingo za bwawa hilo linaweza kustiri miondombinu mingine kama vile ya marabara na umeme.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi