Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Acacia Yachafuka kwa Tuhuma za Rushwa
Oct 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo.

Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatato Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania O’mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara.

Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wakati wa upimaji wa ardhi kwa ajili ya kupanua eneo la mgodi huo.

Vile vile mnamo Machi 7, 2012, Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali, Joseph Thomas Kleruu alipewa tenda ya kufanya tathmini ya shamba Na. 190 lililopo mkoani humo kinyume cha sheria ili kuwasaidia kupata eneo la kupanua mgodi huo.

Imeelezwa kuwa kati ya Januari 2013 na Disemba 2017, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakunguru, Abel Mnyakibari alipewa rushwa ya jumla ya shilingi 966,687,343 kutoka katika mgodi huo ili ajiepushe na kukataa kuwalipa fidia baadhi ya wanakijiji vile vile kati ya Januari 2010 na Disemba 2015, Mwenyekiti huyo alipewa rushwa ya jumla ya shilingi 90,251,475 kwa ajili ya kumshawishi asifatilie fidia ya wanakijiji zaidi ya 800 wa Kijii cha Kewanja.

Kati ya Januari 2006 hadi Mei 2018, Diwani wa Kata ya Kemambo na Mkurugenzi Mtendaji, Bogomba Chichake na Tanzania O'mtima walipewa zabuni ya shilingi 7,709,575,914,19 na shilingi 1,102,880,8 ili kutoihamisha shule ya Nyabigena kutoka eneo la Mrambwe kwenda eneo la Mgema kwa ajili ya kuusaidia mgodi huo kujenga shule kwa bei nafuu.

Kampuni ya Acacia inamiliki migodi mitatu ya dhahabu nchini ikiwemo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, imeandikishwa katika soko la hisa la London. Mnamo Julai 2017, Kampuni hiyo iliipeleka Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi kuhusiana na katazo la kusafirisha makinikia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi