Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Sayi Magessa akifungua kikao kazi cha Kikosi Kazi cha Taifa cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Tanzania kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula jijini Dodoma.
Na WMJJWM- Dodoma
Wizara za Kisekta zimehimizwa kuhakikisha zinatenga Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ili kuweza kutekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Watoto.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idar...