Serikali imezindua mradi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa viwanja vinne vya ndege vya Shinyanga, Tabora, Sumbawanga na Kigoma ili viwe na kiwango cha kimataifa, utakaogharimu shilingi bilioni 136.85.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa viwanja vinne vya ndege vya Shinyanga, Tabora, Sumbawanga na Kigoma, utakaogharimu Sh. bilioni 136.85. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Museum ulioko Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Akizindua ujenz...