Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Rais Dk.Shein Mkoa Kusini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati ) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri jana baada ya kumalizika kwa Mkutano wa majumuisho ya Ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja, uliofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Tunguu Wilaya ya kati Unguja, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mashavu Sukwa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mashavu Sukwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa majumuisho ya ziara yake katika Mkoa wa Kusini uliofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ametoa agizo la kusimamishwa kwa Ujenzi wa majengo katika Kiwanja Kilichokabidhiwa Wizara ya Afya bila ya Serikali kuwa na taarifa rasmi kuhusu Ujenzi huo unaoendelea katika eneo la Binguni Wilaya ya Kati Unguja, awali eneo hilo Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira walilikabidhi kwa Wizara ya Afya,Wizara zinazohusika zimetakiwa kutoa taarifa juu ya Ujenzi unaofanyika katika kiwanja hicho. (Picha na Ikulu.)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama