Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Majaliwa Wilayani Kwimba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya pantoni ya MV Kigongo baada ya kuvuka ziwa Victoria akitoka Sengerema kwenda Kwimba Februari 16, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongell.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo katika mji mdogo wa Ngudu, Februari 16, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Anthony Diallo.

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo katika mji mdogo wa Ngudu Februari 16, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba katika kijiji cha Igumambogo wilayani Kwimba akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Februari 16, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtwika ndoo ya maji, Esther Balele baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Igumambogo wilayani Kwimba Februari 16, 2018.

48 thoughts on “Ziara ya Majaliwa Wilayani Kwimba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama