Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Majaliwa Muleba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (watano kushoto) wakitazama ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti na wanne kushoto ni Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba, DKt. Modest Buchari (kulia) wakati walipokagau ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba (kulia), Oktoba 8, 2018. Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakimjulia hali, Consolata Marios na mwanae Revina Albert wakati walipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Saura Venant na aliyempakata mwanae, Anord Revocatus (kushoto) na Bibi Dorothea Fidel aliyempakata mwanane Redemta Deobey (wapiki kushoto) wakati awalipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa AnnaTibaijuka (mwenye gauni la bluu) wakicheza ngoma ya asili wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba kuhutubiua mkutano wa hadhara, Oktoba 8, 2018.

35 thoughts on “Ziara ya Majaliwa Muleba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama