Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Lukuvi Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori (mwenye suti ya mistari) pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo kuhusu maeneo ya wazi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi yupo jijini Dar es salaam ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo pamoja na viongozi wa wilaya kuhusu maeneo ya wazi katika wilaya hiyo.

Mhe. Lukuvi pia amekutana na Viongozi wa CCM wilaya ya Ilala kuhusiana na changamoto mbalimbali za sekta ya ardhi zinazoikabili ofisi za CCM wilaya ya Ilala.

Aidha Waziri Lukuvi amekutana na watumishi wa Wizara yake waliopewa kazi ya kuhakiki mipaka katika wilaya ya Liwale na wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Wilaya hizi zimekuwa na mgogoro wa mpaka wa muda mrefu unaovikabili vijiji viwili vya Mirui kilichopo Liwale na kijiji cha Nanjilinji kilichopo Kilwa.

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi anataraji kufanya ziara katika wilaya hizo mwishoni mwa wiki hii ili kulitafutia ufumbuzi tatizo la mpaka huu linalozikabili wilaya hizo.


Kikao kati ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo kikiendelea.

. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akiwakaraibisha viongozi wa CCM wilaya ya Ilala katika ofisi yake ya Kanda ya Dar es salaam. Kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Ubaya Salehe Chuma, Mjumbe kamati ya Siasa halmashauri kuu Hemedi Mdeme na Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Joyce Ibrahim.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiongea na viongozi wa CCM wilaya ya Ilala katika ofisi yake ya Kanda ya Dar es salaam.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiongea na viongozi wa CCM wilaya ya Ilala katika ofisi yake ya Kanda ya Dar es salaam.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akiwasikiliza watumishi wa Wizara yake waliopewa kazi ya kuhakiki mipaka katika wilaya ya Liwale na wilaya ya Kilwa.

231 thoughts on “Ziara ya Lukuvi Jijini Dar es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama