Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Zaidi ya Nchi 30 Kushiriki Sabasaba

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw.Edwin Rutageruka akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)

Na: Frank Mvungi

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoanza mapema leo jijini Dar es salaam yakihusisha zaidi ya makampuni 2500 ya ndani na jumla ya nchi 30 zikishiriki.

Kauli hiyo imetolewa Leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade)  Bw. Edwin Rutageruka wakati wa mahojiano maalum kuhusu maonesho hayo.

“Maonesho haya yatafunguliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe mosi Julai 2017 hivyo wananchi wajitokeze ili kushiriki kikamilifu kwa kujionea fursa zilizopo”, alisisitiza Rutageruka.

Aliongeza kuwa katika maonesho hayo kuna siku maalum ya Afrika Mashariki, siku ya ngozi, siku ya asali, zote zikilenga kuhimiza uzalishaji na matumizi ya bidhaa za ndani ili kujenga uchumi wa Viwanda na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Wajasiriamali wadogo wmepewa fursa ykushiriki katika maonesho hayo ili waweze kutangaza bidhaa zao na kubadilishana uzoefu, kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wa nje ya nchi wanaoshiriki maonesho hayo.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) inaratibu na kusimamia maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya kilwa kuanzia June 28 hadi Julai 8,2017.

 

One thought on “Zaidi ya Nchi 30 Kushiriki Sabasaba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama