Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wizara ya Ardhi Yaahidi Ushirikiano Kwa Naibu Katibu Mkuu Mpya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(kulia) ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu ofisini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu (aliyekaa mbele kushoto) na kumkabidhi vitendea kazi leo Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya kukaribishwa kwake katika ofisi za Wizara hiyo leo Jijini Dodoma.Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Naibu wa Wizara hiyo, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) wakifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi zawadi ya ua kwa ajili ya pongezi na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusilukaambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) akimkabidhi zawadi na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) katika hafla fupi ya mapokezi yake na kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka (kulia) leo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Bibi. Dorothy Mwanyika akimpongeza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu mara baada ya kumkaribisha rasmi katika ofisi za wizara hiyo Jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Bibi. Dorothy Mwanyika akimpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Fedha wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Bw. Ndossi wakati wa hafla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu leo Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mthamini Mkuu Tanzania toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Evelyne Mugasha akitoa neno la shukrani kwa na ukaribisho wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu( waliokaa mbele kushoto) na kumuaga aliyekuwa Naibu wa Wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(kulia) leo Jijini Dodoma.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.

Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. John Lupala akitoa neno wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu(kushoto) na kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(mwenye miwani) leo Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi. Dorothy Mwanyika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipongezana na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Mathias Bulugulu mara baada ya kumkabidhi rasmi ofisi na vitendea kazi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Dodoma leo.(Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)

138 thoughts on “Wizara ya Ardhi Yaahidi Ushirikiano Kwa Naibu Katibu Mkuu Mpya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama