Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri wa Fedha Akagua na Kutoa Maagizo Kuhusu Madini ya Almasi Yaliyokamatwa Uwanja wa Ndege

Profesa Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Maalum

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akiangalia Mzigo huo wa Almasi kutoka kwenye kampuni moja ya uchimbaji wa madini hayo Mwadui mkoani Shinyanga, mara baada ya kuhakikiwa na Wataalamu Wazalendo waligundua kuwa mzigo huo una uzito Kg. 29 tofauti na Kg.13 zilizoanishwa na wahusika wa mzigo huo, na thamini yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

3 thoughts on “Waziri wa Fedha Akagua na Kutoa Maagizo Kuhusu Madini ya Almasi Yaliyokamatwa Uwanja wa Ndege

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama