Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Ummy Mwalimu Afungua Mkutano Wa Kifua Kikuu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamad Bakari Kambi(kushoto) na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Motayoba (kulia) kabla ya Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimani Landmark Mjini Dodoma

Baadhi ya waratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma toka Mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mhe.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani)

Mwakilishi wa Mfuko wa Fedha wa Dunia (Global Fund ) toka Geneva Dkt. Osamu Kunii akiongea na waratibu walioshiriki mkutano huo ambapo alisema Tanzania ni nchi ya pili kwa kupata ufadhili mkubwa katika Bara la Afrika ikitangaliwa na Nigeria

Waziri Ummy Mwalimu akihutubia kwenye mkutano huo ambapo aliwasisitiza watoa huduma za afya kote nchini kuweka malengo ya kuwagundua wahisiwa wote takribani laki moja ambao hawajafikiwa ili kuweza kuwakinga watanzania wasipate maambukizi ya kifua kikuu (TB)

Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa mkutano huo. Mkutano huo ni wa siku tatu ambao umeshirikisha mikoa 16 wakiwepo waratibu wa kifua kikuu na ukoma, TAMISEMI, Wadau pamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali (Picha na Wizara ya Afya)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama