Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Prof. Mbarawa Afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Shirika la Posta

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TPC, Joseph Ngowi (kulia), wakati wakimsubiri mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.Wengine kushoto ni Maofisa waandamizi kutoka wizarani.

Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Posta, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Ahmed Kaumo, ambaye pia ni Mwenyekiti TEWUTA, akitoa neno la shukrani kwa Waziri Prof. Mbarawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TPC Dkt. Haruni Kondo akisalimiana na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi mara baada ya kuufungua mkutano wao huo jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, mara baada ya kuufungua mkutano huo, jijini leo. kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.

 

133 thoughts on “Prof. Mbarawa Afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Shirika la Posta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama